JIANDAE KUKUTANA NA MUNGU WAKO!FALME ZA MBINGUNI NA KUZIMU,NA KURUDI KWA KRISTO
Angelica
Zambrano
Imefasiriwa na Alpha Wilson Magubila kwa Neema aliojaliwa na Mungu
Kwa kipindi cha masaa 23, binti mdogo wa ki-Ecuado aitwaye Angelica alioneshwa
falme za
Mbinguni na Kuzimu, na kurudi kwa Kristo mara ya pili. Alishuhudia Yesu akilia
kwa huzuni
aonapo umati wa roho zilizopotea milele, ulimwengu uliomkataa yeye, kanisa lisilo
tayari kabisa
kwa ujio wake, watu wameacha kushuhudia kwa walipotea mbali na kweli, na anasa
za dunia
zimeteka hata watoto kwa shetani. Alishuhudia watu maarufu wakiteswa katika
moto, waimbaji,
wanamuziki na hata Papa. Angelica alioneshwa jinsi ufalme wa Mbinguni
ulivyoandaliwa kwa
uzuri na utayari, utukufu usioweza kufikirika, ambapo hakuna uovu. Japokuwa
Yesu anakuja kwa
ajili ya watakatifu tu; wengi wa wana wa Mungu hawatakuwa tayari kwa siku ile,
na wataachwa
nyuma katika ulimwengu utakaogawanyika vipande vipande.
www.DivineUfunuo.info/23 (Mahojiano
kwa video, mwanzoni ni kwa lugha ya Kihispania, huko El Empalme, Ecuador. Sept.
29, 2009).
Maxima (Mama yake Binti):
Jina langu ni Maxima Zambrano Mora, tunasali kanisa la "Casa de
Oracion" huku El Empalme.
Tulikuwa katika kufunga kwa siku 15, na kulia kwa Mungu. Binti yangu Angelica
aliungana nasi
pia. Katika kipindi hicho cha siku 15 cha kufunga, niliweza kupata maono zaidi
ya asili, ambayo
sijawahi kuona kabla. Tulikuwa tunaomba na kufunga katika kipindi maalumu cha
kumtafuta
Bwana, tuliendelea kuomba na kulia pale nyumbani, tukisubiri Mungu aseme nasi.
Bwana alitutia matumaini makubwa sana. Kwaajili ya majaribu yetu tulikaribia
kukata tamaa,
lakini Bwana alikuwa pamoja nasi kutusaidia. Alitupa neno la Yeremia 33:3
"Niite, nami
nitakuitikia, ame nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.” Binti yangu
alitia
msisitizo sana katika neno hili kwa Bwana, japokuwa sikujua kwa wakati huo.
Angelica (Binti Mhusika):
Jina langu ni Angelica Elizabeth Zambrano Mora. Nina umri wa miaka 18, na
ninasoma chuo cha
"Colegio José María Velazco Ibarra",
hapa El Cantón, El Empalme, Ecuador. Kwanza nilimpokea Kristo nilipokuwa na
umri wa miaka
12, lakini nalijiambia mwenyewe, "Hakuna hata mmoja wa rakifi zangu
aliyeokoka na nikajisikia
aibu miongoni mwao", kwa hiyo nirudi nyuma mbali na Mungu na kuishi maisha
mabaya. Lakini
Mungu alinivuta nitoke huko.
Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 15, nirejea tena kupatana na Bwana, lakini
nia haikutulia sawa
sawa. Biblia inasema (Yakobo 1:8), "Mtu wa nia mbili husita-sita katika
nia zake zote" na mimi
nilikuwa sawa na mtu huyu. Baba yangu aliwahi kusema "Hutakiwi kuwa hivyo,
siyo vizuri, ni
vibaya mwanangu" lakini nalimjibu, "Hivi ndivyo nilivyo, nataka kuwa
hivyo, hakuna mtu wa
kuniambia namna nitakiwavyo kuwa, wala chakufanya, wala namna ya kuvaa, au
mwenendo."
Naye alijibu, "Mungu atakushughulikia na atakubadilisha wewe."
Siku ya sherehe ya kutimiza miaka 17, nilimkaribia Bwana. Tarehe 28 mwezi
Aprili nilimwendea
Bwana na kumwambia, "Bwana, nijisikia vibaya sana, najua kuwa mimi ni
mwenye dhambi” na
nilimweleza jinsi ninavyojisikia. "Bwana, nisamehe mimi. Natamani uandike
jina langu katika
kitabu cha Uzima na unipokee niwe mwanao." Nilitubu na kutoa maisha yangu
kwa Bwana rasmi.
Nikasema “Bwana, naomba unibadilishe, ufanye tofauti ndani mwangu."
Nililia kwa moyo wangu
wote, huku nikimwomba Bwana anibadilishe mimi. Lakini kwa kadri ya muda
ulivyozidi kupita,
sikuona madiliko yoyote. Badiliko pekee nikuwa nilianza kuhudhuria kanisani, kusoma
biblia na
kuomba. Hayo tu ndiyo mabadiliko katika maisha yangu.
Ilipofika mwezi Agosti, nilikaribishwa katika mfungo wa siku 15. Niliamua
kushiriki, lakini kabla
ya kuanza nilisema: “Bwana, naomba unishughulikie hapa." Katika kipindi
chote cha mfungo,
Bwana alikuwa anasema na karibu kila mtu, kasoro mimi tu! Ilikuwa kama vile
Bwana hajaniona,
na hilo liliniumiza sana. Nikaomba, "Bwana, hutanishughulikia mimi?"
Nikaomba na kulia peke
yangu na kusema tena, "Bwana, je unanipenda? Je upo hapa? Upo nami hapa?
Kwanini husemi
nami kama unavyosema na kila mmoja hapa? Unasema mambo mengi kwa wenzangu, hata
maneno
ya unabii, lakini siyo kwangu" Nilimwomba ishara ya kuwa yu nami, na Bwana
akanipa neno la
Yeremia 33:3, "Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa,
magumu
usiyoyajua." Nikasema, “Bwana, je umesema nami?” Kwasababu nilisikia sauti
yake na kupata
maono ya maneno yaliyoandikwa katika Yeremia 33:3.
Nikasema “Bwana, hiyo ni kwaajili yangu?” Nilitunza na kukaa nalo kimya
mwenyewe wakati kila
mmoja akishuhudia waliyopewa na Bwana na kuoneshwa. Lakini mimi nilitunza siri
yangu na mara
kwa mara nilijikumbusha na kutafakari maneno: " Niite" maana yake
nimwombe, lakini nini maana
ya: "mambo makubwa, magumu" niliwaza, “Huenda ikamaanisha Mbinguni na
Kuzimu." Kwa
hiyo nalimwambia “Bwana, naomba unioneshe Mbinguni tu, lakini siyo kuzimu,
kwasababu nimesikia kuzimu ni sehemu ya kutisha na mbaya sana." Lakini
baadaye nikaomba kwa moyo wangu wote, "Bwana kama ni mapenzi yako
kunionesha, na iwe hivyo, lakini nibadilishe kwanza. Naomba ufanye tofauti
ndani mwangu, nataka kuwa tofauti.”
Tulipomaliza kufunga, kulikuwa na majaribu na vipindi vigumu na mara nyingine
nalijisikia kuishiwa nguvu, siwezi tena kuendelea na Bwana. Lakini alinipa
nguvu. Nilianza kusikia sauti yake na kumjua vema zaidi. Tukawa marakifi
wazuri. Bwana ni rafiki yetu mwema, na Roho Mtakatifu pia. Niliwahi mwambia,
"Bwana, wewe ni rafiki yangu bora. Nataka kukujua vema," na
nilishirikiana naye katika mawazo yangu yote.
Nilimwomba kipindi chote cha mwezi Agosti hadi Novemba, na mtumishi wa Bwana
akaja nyumbani kwetu na kusema, "Bwana akubariki." Nikajibu,
"Ameni." Kisha akasema, "Nimekuja kukuletea ujumbe toka kwa
Mungu…...Jiandae, kwasababu Bwana atakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
Atakuonesha wewe Mbinguni na kuzimu kama ulivyokuwa unamwomba neno la Yeremia
33:3." Nikamwuliza, "Ndiyo, lakini umepataje kujua? Sijamweleza
yeyote." Akanijibu, "Mungu unayemtumikia na kumsifu, ndiye nimsifuye,
alinieleza kila kitu."
Mara tukaanza kuomba. Baadhi akina dada toka kanisani kwetu na wana familia
wangu wakaungana nasi kuomba. Lakini mara tulipoanza kuomba, nilianza kuona
Mbingu zikifunguka. Mara nikasema “naona mbingu zikifunguka, na malaika wawili
wanashuka kuja tulipo" Mtumishi wa Mungu akasema “waulize kwanini wamekuja
hapa”
Walikuwa warefu na wazuri wakupendeza; wana mbawa nzuri. Walikuwa wakubwa na
wenye kung’aa, na walionekana wakiangaaza, mng’ao kama wa dhahabu. Walivaa
sandozi za vito vya thamani na walivaa mavazi matakatifu. "Kwanini mko
hapa?" Wakatabasamu na kusema, "Tupo hapa kwasababu tuna kazi
yakufanya….. tupo hapa kwasababu unatakiwa utembelee Mbinguni na kuzimu na
hatutaondoka mpaka yote yatakapo pita." Nikawajibu “safi sana, lakini mimi
natamani kutembelea Mbinguni tu, siyo kuzimu” Wakatabasamu na kuendelea kuwepo
na hawakusema lolote zaidi. Baada ya kumaliza maombi, niliendelea kuwaona
wakiwepo.
Pia nilianza kumwona Roho Mtakatifu; ni rafiki yangu bora; ni Mtakatifu, amejaa
pote na yuko kila mahali wakati wote. Ninamwona, anaangaza na kung’aa sana,
naona tabasamu lake na mtazamo wake wa upendo! Ni vigumu sana kumwelezea, kwa
sababu ni mzuri zaidi ya malaika. Malaika wana uzuri wao lakini Roho Mtakatifu
ni zaidi sana kwa yote. Naweza kuisikia sauti yake, sauti ilijaa upendo na matulizo
makuu. Siwezi kuelezea kabisa sauti yake; kama radi si radi wakati huo huo
yakuvutia. Yeye husema “Niko pamoja nawe” Kwa hiyo nalijitahidi kuendelea
kutembea na Mungu, japo majaribu yalizidi kutuzingira. Tulikuwa tunapita
kipindi kigumu sana, lakini chenye ushindi waajabu. Mie husema “Bwana, mapenzi
yako yatimizwe.” Niliendelea kuwaona malaika wale hata nikiwa shule na pia
darasani. Nilikuwa mwenye furaha ajabu kwa sababu niliwaona vema.
Mtumishi wa Bwana, aliyetutembelea, aliniambia nijiandae, kwa sababu nitakwenda
kuona Mbingu na kuzimu. Lakini pia aliniambia kitu kigumu. Alisema “Nitakufa.”
Haikuwa rahisi niliposikia neno hili.
"Nitakufa namna gani? mie mdogo sana", Nilimuuliza. Akanijibu,
“Usihofu juu ya lolote, Kila kitu Mungu afanyacho hakina makosa wala mawaa, na
atakurejesha duniani, ili utoe ushuhuda juu ya Mbinguni na Kuzimu, kwakuwa hilo
ndilo Bwana anataka sote tujue” Nikasema “Amen, lakini nitagongwa na gari au
nitakufaje?” Mawazo yalinisonga sana, lakini Bwana akaniambia nisihofu, kila kitu
kiko katika uwezo wake. Nikasema, “Ahsante Bwana”
Ilipofika tarehe 6 Novemba, baada ya kurejea nyumbani toka shule, malaika wale
walikuwa nami, hata nilipokuwa namsifu Bwana. Wao walikuwa hawaongei nami; bali
walidumu kusema, “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Hallelujah," huku
wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba wa Mbinguni. Roho Mtakatifu pia alikuwa
na malaika wale huku akifurahi. Watu wengi husema injili/ wokovu ni wa
kuchosha/kukera, lakini huo ni uongo mkubwa toka kwa mwovu ili kuwafanya watu
wasitafute uwepo wa Mungu. Nami pia niliamini hivyo hapo kwanza, lakini baada
ya kukutana na Bwana na Roho Mtakatifu, najua injili haikeri wala kuchosha,
niburudisho la ajabu hapa duniani!
Ninaweza kumwona; kucheza na kuongea naye Roho Mtakatifu. Lakini malaika
walikuwa hawaongei nami, ila walikuwa wakimsifu Bwana. Nikimwambia Roho twende
nami nakufanya hili na lile huja na kuwa nami. Ninaweza kujihisi na kumwona
vema.
Japokuwa wengi hawamwoni, yeye yupo! Mahusiano haya yamendelea, hata hakuna
sababu ya kuyasimamisha, hasa baada ya kuonja radha yake na faida za Roho
Mtakatifu…… hakuna njia ya kujitenga naye jinsi alivyo mwema na wafaida, hasa
nikikumbuka alikonitoa, jinsi nilivyokuwa, ninamshukuru sana kwa rehema zake na
upendo wake kwa wanadamu na kwangu mimi!
Tarehe 7, Novemba, nilipokuwa narudi nyumbani, nikasikia sauti ikisema
“Jiandae, kwakuwa leo utakufa,” Nilijua kuwa ni Roho Mtakatifu kwa vile
nilimwona vema. Niliipuuza sauti yake na kusema “Bwana, Sitaki kufa leo!”
Lakini alirudia, “Jiandae, kwakuwa leo utakufa!” Mara hii sauti ilikuwa ya juu
zaidi na mkazo mkubwa. Nikajibu, “Bwana, najua ni wewe unayesema nami;
nimeuliza ili kupata uhakika tu, mapenzi yako yatendeke. Nitafanya kila utakalo
niambia, najiachia kwako Bwana, japo naogopa, najua upo nami, nawe ni wa
kweli.” Niliomba, “Bwana, Yule mtumishi wako uliyemtumia kunipa ujumbe mara ya
kwanza, mlete muda huu, nimkute nyumbani, na umpe tena neno hili aseme nami
kuwa leo ndiyo siku yangu ya kufa.” Sasa mara zote Bwana hujua ya nyuma,
yaliyopo na yajayo. Alijua kuwa nitamwomba neno hili. Kwa hiyo nilipofika
nyumbani nikamkuta mtumishi wa Bwana ameishafika!.
Maxima (Mama ya Binti):
Binti yangu alipofika nyumbani, tulikuwa jikoni. Mara Angelica alipomwona
mtumishi wa Bwana, akasema, “Bwana akubariki.” Mtumishi wa Mungu akajibu,
“Bwana akubariki nawe. Je uko tayari? Kwa kuwa leo ndiyo siku Bwana atakayo
kuchukua, saa kumi jioni.” Angelica alisimama na kushikwa na mshangao kwamba
Bwana amejibu ombi lake na kufanya vilevile alivyomwomba njiani.
Angelica:
Niliposikia hayo maneno ya mtumishi, nikasema, “Ameni... lakini sitaki kufa,
sitakufa! Hapana, Bwana, naogopa, naogopa sana, ninahofu kubwa!” Mtumishi wa
Bwana akasema, “Tuombe ili hofu ikutoke sasa kwa jina la Bwana.” Nikasema,
"Ameni" na tukaomba. Ghafla nikajisia hofu yote imenitoka na furaha
isiyoelezeka ikajaa ndani mwangu, nakuanza kuwaza kuwa kifo ni kitu chema
kuliko vyote nikitamanicho kinifike! Nikanza kutabasamu na kicheka wakati huo
kila mmoja
aliyepo akinitazama. Wakaniona jinsi nilivyobadilika toka unyonge na kuwa
mwenye furaha.
Nilikuwa natabasamu, narukaruka na kuimba.
Picha wakimwombea:
Maxima:
Binti yangu ghafla akawa mwenye furaha ndani ya moyo na kuanza kula. Alionja
karibia kila kitu
kilichokuwepo, huku akisema, “Kama sitarudi, sawa nimeshakula na kushiba.”
Angelica:
Kila mmoja akaanza kucheka na kuuliza, “kwanini uko hivyo badala ya kuwa na
huzuni, unafuraha
na mwenye raha?” nikawajibu, “Ndiyo ninafuraha: ninakwenda kumwona Bwana,
nitakuwa naye,
lakini sijui kama nitarudi. Kwa hiyo nataka kugawa vitu vyangu vyote.” Wote
wakastaajabu na
kuniuliza, “Unataka kugawa vitu vyako vyote?” macho ya mama yangu yalinitazama
kwa
mshangao zaidi!
Maxima:
Binti yangu akaanza kugawa vitu vyake. Aligawa vyote, vyote! Ma-dada wa
kanisani walikuwepo,
nao pia aliwapa baadhi ya vitu kwa kila mmoja. Nilipomuuliza nia yake, alisema,
“Kama nikirudi,
watanirejeshea vyote, lakini nisiporudi, watabaki navyo.”
Angelica:
Niliwaza huzuni aliyokuwa nayo mama yangu niliposema maneno hayo. Lakini
nilijisikia furaha
tupu, kwa hiyo nikaendelea kugawa vitu: nguo, kitanda, simu ya mkononi, kila
kitu, lakini kwa
sharti: kama nikirudi, kila kitu kitarejeshwa kwangu. Wote wakaanza kucheka.
Maxima:
Binti yangu alikuwa na msimamo na nia ya dhati, lakini kama mama nilishikwa na
huzuni sana.
Haikuwa jambo rahisi. Niliwaza, “Bwana muda huo ukiwadia, itakuwajekuwaje?”
Sikuweza
kuelewa. Na walipoanza kuomba, nilikuwa napanga vitu ndani ya nyumba. Walisema,
“Dada njoo
tuombe.” Lakini niliwajibu, “Nyie endeleeni, nitajiunga nanyi muda si mrefu.
Ngoja nimalizie kazi
hii.”
Angelica:
Wote walikuwa wananiangalia mimi tulipokuwa tunaomba. Niliomba, “Bwana, nataka
kufanya
mapenzi yako. Wewe si mwanadamu hata useme uwongo au ujute, najua wewe ni
mkweli. Kama
nitakuaibisha, basi vema unichukue moja kwa moja; lakini kama nitayafanya
mapenzi, basi
unirejeshe tena, lakini nisaidie kusema ukweli, niandae mimi, nisaidie kuhubiri
na kuwaambia watu
kutubu.” Hiyo ndiyo ilikuwa sala yangu fupi sana. Nilimwambia mtumishi wa
Bwana,
“Usimwambie mama yangu maneno niliyomwomba Bwana.” Naye akajibu, “sitamwambia
sasa,
lakini mara Bwana atakapokutwa, nitamwambia.” Tuliendelea kuomba na kuungana
katika duara.
Maxima:
Ilipofika saa 9:30 jioni, Bwana akamwambia mtumishi wake ampake mafuta binti
yangu. Kwa hiyo
baadhi yetu tulikwenda chumbani na kumpaka mafuta. Alitupa dakika mbili tumpake
mwili mzima,
toka kichwani hadi chini, kila mahali, mwili mzima. Akawa mwili wote amepakwa
mafuta.
KIFO CHAKE
Angelica:
Mama yangu na dada mmoja, Fátima Navarrete, walinipaka mafuta. Kadri
walivyokuwa
wananipaka, nilijisikia kama kuna kitu kinanifunika, kama kioo kilinizunguka
mimi. Ni vigumu
kuelezea, nilijisikia kama nimezingirwa na ngao fulani, na nashindwa kuelezea
nilivyokuwa
najisikia. Baada ya hapo kila walipojaribu kunigusa walishindwa!
Maxima:
Kadri tulivyokuwa tukimwombea Angelica, nilijaribu kuweka mkono juu yake,
nilishindwa!
Alikuwa amezingirwa na kitu. Ilikuwa ajabu, hakuna aliyeweza kumgusa tena! Uzio
huo ulianzia
kichwani hadi miguuni, karibia sentimenta 30 (Inchi 12). Hilo lilinitisha zaidi
mimi. Nimewawekea
mikono wengi kabla, katika huduma ya Bwana, lakini jambo kama hili halijawahi
kutokea!
Nikasema, “Oh, kuna jambo lazima linatendeka,” na nikaanza kuomba na kumshukuru
Bwana.
Ghafla, nikasikia furaha kubwa sana. Huzuni iliyokuwa moyoni ikanitoka, maumivu
yakakoma na
sasa nikasikia raha na furaha ajabu! Tuliendelea kuomba na ilipofika saa 10.00
jioni, binti yangu
akaanguka sakafuni.
Angelica:
Wakati wa maombi, nilisikia kuishiwa pumzi; nikashindwa kupumua. Nikasikia
maumivu tumboni
na moyoni. Nilijisiki damu ikisimama, na ghafla maumivu makali mwili mzima.
Nililoweza
kusema, “Bwana, nipe nguvu, nipe mimi nguvu!” kwasababu nilijisikia kushindwa
kuendelea zaidi.
Sikuwa na nguvu kabisa, zote zilinitoka! Na nilipoangalia juu mbinguni, katika
roho, si kwa macho
ya mwilini, niliona mbingu zikifunguka. Niliwaona malaika, siyo wawili au kumi,
bali kwa
mamilioni wakiwa pamoja wamekusanyika. Katikati yao niliona mwanga, mara 10,000
zaidi ya
jua. Na nikasema, “Bwana ni wewe unayekuja!”
Maxima:
Alipoanguka chini, tulijaribu kumsimamisha, lakini hakuweza kusimama mwenyewe.
Muda huu
tuliweza kumgusa. Alikuwa akisema, “Omba. Sina nguvu, mama, sina nguvu na
ninasikia
maumivu.” Mwanzo alisikia maumivu tumboni, na baadaye moyoni. Tuliendelea kuomba
na
kumsihi Bwana. Bwana alichukua maisha yake!
Picha Mwili wake:
Sijawahi katika maisha yangu kumwona mtu akifa. Nilishuhudia binti yangu,
akigugumia maumivu! Haikuwa rahisi hata kidogo! Sikuweza kuelewa maneno yake ya
mwisho, na mwisho alitulia. Niliweka mikono yangu usoni pake, na kioo mdomoni
kuona kama alikuwa anapumua. Hakuwa na pumzi tena, alitulia kimya kabisa.
Nilimshika, alikuwa angali na joto kama kawaida. Nilichukua shuka na kumfunika
na kwa muda mfupi akaanza kupoa na kuwa wa baridi sana. Nywele zake zikalala,
kama za maiti na akabadilika ubaridi wa barafu.
Angelica:
Yesu alikuwa anashuka chini, na nikajisikia mwili ukifa. Kadri Yesu na malaika
walivyozidi kukaribia, nikajisikia kuondoka, na sikuwa mimi tena. Sikuwa hai
tena, nilikuwa nakufa na kugugumia maumivu! Wakati mwili wangu ulipoanguka
chini, walikuwa tayari wamefika. Nyumba yetu ilijaa malaika, na katikati yao
niliona mwanga mkali kuliko wa jua! Ilikuwa vigumu; nilisikia maumivu makali
wakati roho yangu ilipotenganishwa na mwili. Nilikuwa nalia na kupiga kelele,
kadri nilivyoona mwili wangu sakafuni. Nilimuuliza, “Bwana, nini kinachotokea?
Nini kinachotokea?” Nilijaribu kuugusa mwili wangu na kuurudia tena, lakini
nilipojaribu, ilikuwa kama kushika hewa: sikuweza kuugusa, mkono wangu
ulipitiliza. Hakuna kati ya waliokuwa wananiombea aliyenisikia! Na nikapiga
kelele, “Bwana, nisaidie mimi!”
Maxima:
Mume wangu alifika tulipokuwa tunaomba, na alimkuta pale. Bwana alinipa nguvu
kwa kuwa sikujua la kufanya. Ilikuwa kama vile yuko mahututi (kwenye coma),
lakini nilijua yuko salama, kwasababu ilikuwa ni kazi ya Bwana. Kwahiyo
nikasema “Bwana, mapenzi yako yafanyike.”
BWANA YESU KRISTO
Angelica:
Wakati huo nasikia sauti ya Bwana, sauti nzuri kama radi lakini ya UPENDO,
“Usiogope, Binti, kwa kuwa mimi ni Yehova, Mungu wako, na nimekuja hapa
kukuonesha niliyokuahidi wewe. Inuka, kwa kuwa mimi ni Yehova, ninayekushika
mkono wako wa kuume na kukuambia, usiogope, nitakusaidia wewe." Ghafla,
nikasimama. Nilikuwa nimepiga magoti chini, ninauangalia mwili wangu, nikitaka
kuurejea bila mafanikio. Niliposikia sauti yake, woga ukanitoka, na sikuwa na
hofu tena. Nilipoanza kutembea, malaika wakaanza kufungua njia. Kulikuwa na
mwanga mkali ung’aao, na nilipouangalia nilisikia amani ya ajabu. Kadri nilivyoangalia,
nilimwona mwanaume mzuri, mrefu, aliyevaa vizuri na kuvutia sana kumwangalia,
mwenye siha njema. Mwanga ulitoka kwake. Kulikuwa na mwanga mkali kiasi cha
kushindwa kumwangalia uso wake! Lakini niliweza kuona nywele zake za dhahabu
ing’aayo na vazi jeupe na mshipi kifuani pake. Ukisomeka, “MFALME WA WAFALME NA
BWANA WA MABWANA.”
Nilimwangalia miguuni pake, alikuwa amevaa sandozi zenye mng’ao wa dhahabu,
dhahabu safi. Alikuwa mzuri sana! Akaninyooshea mkono wake. Nilipomshika mkono
wake, haikuwa kama nilipojaribu kuugusa mwili wangu, mkono haukupitiliza.
Nikauliza, “Nini kinachotokea?” naye akasema, “Nitakuonesha wewe kuzimu ili
ukirudi uwaambie wanadamu kuwa kuzimu ni halisi; kuwa ni kweli ipo. Na pia
utukufu wangu nitakuonesha wewe, ili uwaambie watu wangu wajiaandae, kwa kuwa
utukufu wangu ni halisi na mimi pia.” Akasema, "Binti, usiogope” akarudia
kusema tena na mimi nikasema, "Bwana, nataka tu kwenda Mbinguni, lakini
siyo kuzimu, kwasababu nimesikia kunatisha!” Akasema, “Binti, nitakuwa nawe.
Sitakuacha huko na nitakuonesha huko mahali kwasababu wengi wanajua kuzimu ipo
lakini hawaiogopi.
Wanaamini ni mchezo, na kuzimu ni mzaha, na wengi hawajui lolote juu yake.
Ndiyo maana
nitakuonesha wewe huko kwa sababu wanaopotea ni wengi kuliko wanaoingia katika
utukufu
wangu.” Aliposema hayo, niliona machozi yakitiririka kwenye vazi lake.
Nikamwuuliza, “Bwana,
kwanini unalia?” Akanijibu, “Binti, kwasababu wengi wanaangamia, na
nitakuonesha hii, ili
uende na uwaambie ukweli na wewe usirudie hapo.”
KUZIMU
Ghafla, alivyokuwa anaongea, kila kitu kikaanza kutembea. Ardhi ilitikisika na
kupasuka, na
nikaona shimo jeusi tii chini.
Shimo:
Tulikuwa tumesimama kama kwenye mwamba na malaika wakituzunguka. Nikasema,
“Bwana,
sitaki kwenda mahali huko!” akasema, “Binti, usiogope niko pamoja nawe.” Kwa
sekunde chache
tukashuka kwenye shimo jeusi. Nilijaribu kuangalia lakini kulikuwa na kiza
kikuu. Niliona duara
kubwa, na kusikia mamilioni ya sauti.
Nilipata moto. Nikajisikia ngozi yangu kuungua. Nikamuuliza, “Bwana, hiki ni nini?
sitaki
kwenda mahali huko!” Bwana akasema hilo ni lango tu la kwenda kuzimu. Kulikuwa
kuna harufu
mbaya, yakutisha, isiyovumilika, na nikamsihi Yesu asinipeleke mimi. Naye
akajibu, “Binti, ni
muhimu ufike na kujua sehemu hii.” Nikalia, “Lakini kwanini, Bwana, kwanini?”
naye akasema,
“Ili ukawaambie ukweli wanadamu; wanadamu wanaangamia, wanapotea na wachache
sana
wanaoingia ufalme wangu.” (Mat.7:14) Akishasema hivi, hulia sana. Maneno yake
yalinitia nguvu
na kunihimiza, kwa hiyo nikaendelea kutembea.
Ziwa la Moto:
Tulifika mwisho wa tanuru/lango, nilipoangalia chini niliona umati umefunikwa
na miali ya moto. Bwana akasema “Binti, nakupa hii.” Ilikuwa ni faili kubwa
lenye karatasi ambazo hazijaandikwa chochote. “Binti, chukua na kalamu hii ili
uweze kuandika yote nitakayokuonesha, utakayoyaona na kusikia. Utaandika kila
kitu ukionacho na utaishi nayo.” Nikasema, “Bwana, nitafanya, lakini
nimeshaanza kuona mengi mno, Bwana. Ninaona roho zikiteswa, na kuzamishwa
kwenye moto.”
Maxima:
Muda uliendelea kupita, na binti yangu alikuwa bado kalala pale. “Bwana, nini
kinachotokea?” Machozi yalikuwa yakimtoka kwenye macho, lakini kila
nilipomfuta, yalitoka tena. Nikaweka kioo mdomoni pake kuona kama anapumua,
hakukuwa na pumzi. Tuliangalia mapigo ya damu, wapi, hakuna kitu!. Tuliweka
mikono tumboni pake, wapi! Hakuna kitu. Mtumishi wa Bwana akasema, “mahali
alipo sasa, siyo mahali pa kutabasamu bali mahali pa mateso.”
Angelica:
Nikamwambia Yesu, Nitashuhudia kuwa kuzimu ni halisi, kwamba ipo, lakini nitoe
hapa sasa!” na akanijibu, “Binti, hatuja ingia bado mahali penyewe, na
sijakuonesha chochote, tayari unataka nikutoe huku?” nikasema “Bwana, tafadhari
nitoe mahali hapa,” tukaendelea kushuka kwenye korongo/shimo lakutisha!
Nikaanza kulia na kupiga yowee, “Bwana, hapana, hapana, hapana, hapana………
Sitaki kwenda!” naye hujibu, “Unatakiwa kuona haya.”
Niliona mapepo yakutisha, ya kila aina, makubwa na madogo. Yalikuwa yanakimbia
sana, na yameshika vitu mkononi. “Bwana, kwanini yanakimbia hivyo na yameshika
nini?” akanijibu, “Binti, wanakimbia hivyo kwasababu wajua muda wao karibu
kwisha, kwasababu muda wa kuwaharibu/kuwapoteza wanadamu, hususani watu wangu.
Na walivyoshika mkononi ni mishale ya kuwaharibu wanadamu, kwasababu kila pepo
amepewa jina na kwa kadri ya jina lake, ana mishale ya kumharibu mtu na kumleta
huku kuzimu; malengo yao ni kumharibu mtu na kumleta kuzimu.” Na niliendelea
kuona mapepo yakikimbia na kutoka kuelekea duniani na Bwana akaniambia;
“Wanakwenda duniani ili kuleta na kuwatupa wanadamu huku." Alipokuwa
akisema hivyo, Bwana hulia, hulia sana. Kila alipolia nami nililia pia.
Maxima:
Binti yangu alikuwa amekufa kwa masaa 23, lakini sikutoa taarifa kwenye mamlaka
yoyote. Niliomba, “Bwana, nitasubiri kwa masaa 24. Kama binti yangu hatarudi
ndani ya saa 24, nitampigia simu Daktari.” Lakini, Bwana alimrejesha kabla ya
saa 24 hazijatimia.
Angelica:
Bwana akaniambia, “je uko tayari kuona nitakachokuonesha wewe?” Nikasema,
“Ndiyo Bwana,”. Alinipeleka kwenye sero moja, ambapo nilimwona kijana akiwa
matesoni katikati ya miali ya moto. Nikajulishwa namba sero yake, japokuwa
sikuweza kujua ile namba, ilionekana kama imeandikwa kinyume hivi. Palikuwa na
nembo kubwa mle ndani, na kijana alikuwa na namba 666 kwenye kipaji cha uso.
Pia alikuwa na aina ya kipande cha chuma imebandikwa kwenye ngozi yake. Funza
walikuwa wanamtafuna, haikuweza kuharibu kipande kile; wala moto haukuweza
kukiunguza. Akapiga kelele, “Bwana, nirehemu mimi. Nitoe mahali hapa. Nisamehe
mimi Bwana!” lakini Yesu alimjibu, “umechelewa, umechelewa sana: nilikupa fursa
lakini hutaka kutubu.” Nikamuuliza Yesu, “Bwana, kwanini huyu yuko hapa?” mara
nikajulishwa.
Akiwa duniani, kijana huyu alijua neno la Mungu, lakini ghafla akajitenga na
Bwana na kuchagua
pombe, madawa ya kulevya na kupita katika njia zisizofaa. Hakutaka kufuata njia
ya Bwana. Yesu
alimwonya mara nyingi juu la litakalompata. Yesu akasema, “Binti, yuko hapa
kwasababu kila
anayeyakataa maneno yangu, anaye amhukumuye: lile neno nilisema naye
litamhukumu siku
ya mwisho,” (Yohana 12:48) na Yesu akalia tena.
Bwana akilia, nitofauti nasi tuliavyo na zaidi yetu. Yeye hulia na maumivu
makali moyoni na
uchungu usioelezeka. Bwana akasema, "Sikutengeneza kuzimu kwaajili ya
wanadamu,”
Nikamuuliza, “Sasa Bwana kwanini wanadamu wapo huku,” Akanijibu, “Binti,
niliumba kwajili
ya shetani na malaika zake, ambayo ni mapepo;(Mat. 25:41) lakini, kwasababu ya
dhambi na
kukosekana kwa toba, wanadamu huishia hapa, na wengi wangamiao kuliko wanaofika
katika
utukufu wangu!" Akaendelea kulia na huniumiza sana nimwonapo akilia.
"Binti, nalitoa maisha
kwaajili ya wanadamu, ili wasiangamie, ili wasiishie hapa [Kuzimu]. Nalitoa
maisha yangu kwa
upendo na huruma, ili wanadamu waendee toba na kuingia katika ufalme wa
Mbinguni.” Yesu
kwa huzuni huugua kiasi cha kushindwa kustahimili maumivu, kadri aonavyo watu
pale kuzimu.
Kwa kuwa na Yesu, kulinifanya nijisikie salama. Niliwaza, “kama nikimwacha
Bwana aende,
ninge-nasa kuzimu pale” Nikamuuliza, “Yesu, je nina ndugu yangu mahali hapa?”
Akanitazama
kwa jinsi nilivyokuwa nalia na akasema, “Binti, niko nawe,” Kwasababu nilikuwa
mwenye hofu
sana. Akanipeleke kwenye sero nyingine. Sikuwahi kuwaza kumwona ndugu yangu
kwenye sero
ile. Nilimwona mwanamke akiteswa, alikuwa na funza wakimla uso wake, na mapepo
yakimchoma
mikuki mwilini. Naye hupiga kelele, “Hapana, Bwana, nihurumie, nisamehe mimi,
tafadhari, nitoe
mahali hapa kwa dakika moja!” (Luka 16:24)
Kuzimu, watu huteswa na kumbukumbu za waliyoyafanya duniani. Mapepo hudhihaki
watu na
kuwaambia, “abudu na kusifu kwasababu huu ndiyo ufalme wenu!” na watu hupiga
kelele
11
wakikumbuka kuwa walimjua Mungu, kwasababu walijua neno. Walimjua Bwana
waliteswa mara
dufu ya wengine.
Bwana akasema, “Hakuna tena nafasi kwa walioko pale[kuzimu]; kungali na nafasi
kwa walio
hai.” Nikamuuliza, “Bwana, kwanini bibi yangu mkubwa yupo pale? Sijui kama
alikujua wewe.
Kwanini yupo kuzimu Bwana?” akanijibu, “Binti, yupo hapa kwasababu alishindwa
kusamehe….. binti, yeyote asiyesamehe, sitamsamehe huyu.”
Nikamuuliza, “Bwana, lakini wewe husamehe, na una rehema.” Naye akanijibu,
“Ndiyo, binti,
lakini nilazima kusamehe, kwasababu hawajawasamehe wengi, na ndiyo maana wengi
wapo
hapa, wameshindwa kusamehe…… nenda kawaambia wanadamu ni muda wa kusamehe, hasa
hasa watu wangu, kwakuwa wengi miongoni mwa watu wangu hawajasamehe. Waambie
waache malaaumu, mafundo, chuki mioyoni mwao, kwa kuwa ni muda wa kusamehe!
Kama
kifo kikimsitukiza mtu aliyeshindwa kusamehe, huyo mtu atakwenda kuzimu,
kwakuwa hakuna
awezaye kununua maisha.” Tulipoondoka hapo, bibi yangu mkubwa alifunikwa na
moto na
akapiga makelele, "Aaaah," na akaanza kutukana jina la Mungu, na
kumlaani Bwana; kila mtu
kuzimu humtukana Mungu.
Tulipoondoka eneo lile, nikaona kuwa kuzimu imejaa roho ziteswazo. Watu wengi
huinua mikono
nje, wakimwomba Yesu msaada wa kuwatoa nje. Lakini Bwana hakuwa na lolote la
kufanya kwao,
nao huanza kumtukana Mungu. Mara Yesu hulia sana na kusema, “Inaniumiza sana
kuwasikia,
inaniumiza mimi sana wanavyofanya, kwasababu siwezi kufanya lolote kwaajili
yao. Ninacho
kueleza ni hiki; nina nafasi kwa hao walioko duniani, ambao hawaajafa, walio
hai, wanao muda
wa kutubu!”
Bwana akaniambia kuna watu wengi maaruku huku kuzimu, na pia wengi waliomjua
Bwana.
Akasema, “Nitakuonesha upande mwingine wa tanuru.” Tukaenda mahali penye
mwanamke
aliyezingirwa na miali ya moto. Alikuwa katika maumivu makubwa na kupiga
makelele, akiomba
huruma kwa Bwana. Yesu akanyoosha mkono kwake na akaniambia, “Binti, Yule
mwanamke
umwonaye pale, amezingirwa na miali ya moto ni Selena.” Kadri tulivyokuwa
tunamkaribia,
akapiga kelele, “Bwana, nihurumie mimi, nisamehe mimi Bwana, nitoe mahali
hapa!” lakini
Bwana akamtazama na kusema, "Umechelewa, umechelewa sana, huwezi kutubu
sasa.”
Selena
Aliponiona mimi akasema, “Tafadhari, nakuomba wewe, waambie watu hivi, tafadhari
sema na
usinyamaze; nenda waambie wasije mahali hapa; nenda waambie wasisikilize nyimbo
zangu, wala
wasiimbe hizo nyimbo.”(1 Yohana 2:15) Nikamuuliza, "kwanini unataka mimi
niwaambie hivyo?"
naye akanijibu, "Kwasababu kila wakati watu wanaposikiliza nyimbo zangu,
nateswa zaidi na
zaidi, na mtu anayeimba na kusikiliza nyimbo zangu, anaelekea mahali hapa.
Tafadhari, nenda
uwaambie wasije huku; nenda waambie kuzimu ni halisi, ipo kweli!”. Akapiga
kelele na mapepo
humchoma mikuki na Selena kulia, “Nisaidie mimi, nihurumie mimi Bwana!” lakini
kwa huzuni
Bwana alimwambia, “umechelewa sana.”
Nikaangalia pande zote za eneo lile, lilikuwa limejaa waimbaji na wasanii
waliokufa. Walikuwa
wakiimba na kuimba, bila kusimama. Bwana akanifafanulia, “Binti, mtu aliyepo
hapa, lazima
aendelee kufanya kile alichokuwa anafanya duniani, kama hajatubu."
Kadri nilivyokuwa naangalia eneo lile, niliona mapepo mengi yakinyunyiza vitu
kama mvua.
Nilidhani ni mvua inanyesha. Lakini niliona watu kwenye miali ya moto
wakikimbia mbali na ile
mvua na kupiga yowee, “Hapana, nisaidie, Bwana!..... Hapana, haiwezekani kuwa
hivyo,” na
mapepo yalikuwa yanacheka na kuwaambia watu, “Sifu na kuabudu kwasababu hapa ni
ufalme
wenu milele na milele!” Niliona miali ya moto ikiongezeka na funza za watu
zikiongezeka zaidi!
Hayakuwa maji yale bali kiberiti cha kuongeza miali ya moto na kuongea maumivu
ya kila mtu.
Nikamuuliza Yesu, “Ni nini kinachotokea?..... Bwana, ni nini hiki?” Bwana
akanijibu, “Huu ni
ujira wa yeyote asiyetubu.” (Zaburi 11:6).
Bwana akanipeleka mahali alipo mtu aliyejulikana sana. Kabla ya maono haya,
nilishi maisha kama
msichana wa kikristo wa nia mbili. Nilidhani kila mtu anayekufa anakwenda
Mbinguni; wale
walifanyiwa ibada za mazishi watakwenda mbinguni, kumbe sikuwa sahihi, nilikosa.
Alipofariki
Papa John Paul II, marafiki zangu na ndugu walisema amekwenda mbinguni. Taarifa
zote kwenye
LUNINGA [TV], na vyombo mbalimbali vya habari vilisema, "Papa John Paul II
amefariki,
apumzike kwa amani. Anafurahia sasa kuwa na Bwana na malaika Mbinguni" na
mimi niliamini
yote kuwa ndivyo. Lakini kumbe nilikuwa najidanganya mwenyewe, kwasababu
nimemwona
kuzimu, akiteswa kwa miali ya moto. Nilimtazama uso wake, alikuwa mwenyewe Papa
John Paul
II! Bwana akaniambia, “Angalia, Binti, Yule mwanaume umwonaye pale, ni Papa
John Paul II.
Yuko hapa; akiteswa kwasababu hakutubu.”
Papa John Paul II
Lakini nikamuuliza, “Bwana, kwanini yuko hapa? Alikuwa akihubiri kanisani.”
Yesu akanijibu,
“Binti, hakuna mwasherati, wala muabudu sanamu, hakuna mchoyo na hakuna mwongo
atakayerithi ufalme wangu.” (Eph 5:5) Nikamjibu, “Ndiyo, najua ni kweli, lakini
nataka kujua
kwanini yuko hapa, kwasababu alikuwa akiwahubiria umati wa watu!" Na Yesu
akanijibu, “Ndiyo,
Binti, alisema mengi, lakini hakusema kweli kama ilivyo. Hakusema kweli na
kweli aliijua na
japokuwa aliijua kweli, alipenda fedha zaidi ya kuhubiri habari za wokovu.
Hakutoa uhalisia;
hakusema kuzimu ni halisi na mbinguni kupo; Binti, sasa yuko mahali hapa."
Nilipomwangalia mtu huyu, alikuwa na joka kubwa lenye sindano nyingi mwilini
mwake, limemzingira shingoni, naye hujaribu kumtoa. Nalimwomba Yesu, “Bwana,
msaidie!” Mwanaume hupiga kelele, “Nisaidie mimi, Bwana nihurumie; nitoe mahali
hapa; nisamehe mimi! Ninatubu Bwana; Nataka nirudi duniani, nataka nirudi
duniani nikatubu.” Bwana alimtazama na kumwambia, “Ulijua vizuri yote haya.
Ulijua vema kuwa kuzimu ni halisi, ipo…….. umechelewa; hakuna tena nafasi
kwaajili yako.”
Bwana akasema, “Tazama Binti, nitakonesha maisha ya mtu huyu.” Yesu akanionesha
kioo kikubwa kama LUNINGA [TV]; nikaona alivyotoa misa mara nyingi kwa umati wa
watu. Na watu wale walivyokuwa waabudu sanamu. Yesu akasema, “Tazama, Binti,
wapo waabudu sanamu wengi hapa [Kuzimu]. Ibada ya sanamu haiwezi kuokoa Binti.
Ni mimi pekee niwezaye kuokoa, na nje yangu hakuna mwingine aokoaye. Nawapenda
wenye dhambi, lakini nachukia dhambi Binti. Nenda na uwaambie wanadamu kuwa
nawapenda na ninataka waje kwangu.”
Kadri Bwana alivyokuwa akisema, nilianza kuona mtu huyu akipokea makusanyo
makubwa ya sarafu na fedha; vyote alivihifadhi. Alikuwa na fedha nyingi sana.
Naliona sura yake imeketi katika mamlaka yake, lakini pia naliweza kuona zaidi.
Japo ni kweli watu hawa hawaoi, ninakuhakikishia wewe, sizushi, Bwana
alinionesha mimi, wanalala na masista; na wanawake wengi!
Bwana akanionesha watu hawa wanaishi kwa uasherati, na neno linasema hakuna
mwasherati atakayerithi ufalme wake. Kadri nilivyokuwa naona, Bwana akaniambia,
“Tazama, Binti, yote ninayokuonesha, ndiyo yanayoendelea, ndivyo alivyoishi
[Papa] na ndivyo yanayotokea katikati ya watu wengi, katikati ya mapadre na
mapapa waliopo.” Kisha Bwana akasema, “Binti, nenda na uwaambie wanadamu ni
muda wa kugeukia.”
Bwana akanionesha sehemu watu wengi wanavyoelekea kuzimu. Nikamuuliza, “Bwana,
namna gani wanakuja huku?” akanijibu, “Nitakuonesha.” Akanionesha lango lenye
watu wengi wakipita. Watu hawa walikuwa wamefungwa toka mikononi hadi miguuni.
Walivaa mavazi meusi na kubeba mizigo mgongoni mwao. Yesu akasema, “Binti, hao
watu uwaonao hawanijui mimi bado. Mizigo waliyobeba ni dhambi, lakini nenda
waambie walete mizigo kwangu, nami nitawapumzisha; kwa kuwa mie ndiye mwenye
kusamehe dhambi zao zote…. Binti, nenda na uwaambie waje kwangu, kwani
nawasubiri na mikono yangu iko wazi kuwapokea, na uwaambie hapo wanaelekea
mahali hapa [kuzimu].”
Kadri nilivyokuwa nawatazama watu wakitembea, nikamwambia, “Bwana, Yule mtu
pale ni binamu yangu; na Yule kijana pia, Bwana, na Yule binti pale anayelekea
kuzimu; oh familia yangu inakuja huku kuzimu!” Bwana akajibu, “Binti, wanakuja
huku, lakini nenda uwaeleze wanakoelekea, nenda waeleze kuwa wanakwenda kuzimu.
Nenda waeleze kuwa nimekuchagua wewe uwe mlinzi wangu…… nimekuchagua wewe kama
mlinzi, hii inamaanisha kuwa unatakiwa uwaambie ukweli. Unatakiwa uende
uwaeleze yote niliyokuonesha wewe. Kama hutawaambia na jambo likampata mtu
huyu, damu yake itakuwa juu yako, lakini ukiende na kufanya nilivyokueleza,
hapo mtu huyu nitamdai mwenyewe. Kama mtu hatatubu, hapo wajibu ulionao
utaondolewa, kwa kuwa atadaiwa mwenyewe na damu yake haitakuwa juu yako.
(Ezekia 3:18)"
Yesu akaniambia wengi wa watu maarufu wanaelekea huku [kuzimu], maarufu na watu
muhimu. Kwa mfano, Michael Jackson. Huyu alikuwa maarufu duaniani kote lakini
alikuwa mjumbe wa
shetani. Japokuwa wengi wanaweza wasione na kuelewa hivyo, lakini huo ndiyo
ukweli. Huyu
alikuwa na mkataba na shetani: alikubaliana na shetani ili awe na heshima na
sifa ilikuwa vutia
wapenzi wengi.
Michael_Jackson
Hizo hatua na mitindo aliyokuwa anafanya, ndivyo nilivyoona mimi mapepo
yakicheza na
kutembea yanapotesa watu kuzimu. Yalikuwa yanateleza kwa kurudi nyuma na siyo
mbele, huku
yakipiga kelele; yakifurahia mateso wanayopata watu. Ngoja nikuambia wewe kuwa
Michael
Jackson yuko kuzimu. Bwana alinionesha baada ya kufa Michael. Alinionesha Michael
Jackson
akiteswa kwenye miali ya moto. Nikalia kwa Yesu, “Kwanini?” haikuwa rahisi
kuona mtu huyu
alivyokuwa anateswa na alivyokuwa analia na kupiga mayowe. Yeyote anayesikiliza
nyimbo za
Michael Jackson au kuziimba au ni mpenzi/shabiki wa Michael Jackson, ninakuonya
kuwa shetani
anakutega katika mtego wake ili mwisho uishie kuzimu. Mara hii, jitoe na
kumkana shetani kwa
jina Yesu! Yesu anataka kukuweka huru wewe, ili usipotee milele. Bwana
akaniambia, “Binti,
kuna watu wanijuao pia wanakuja huku.” Nikamuuliza, “Bwana, inakuwa je mtu
akujue harafu
aje huku?” akanijibu, “Mtu Yule aliyeacha njia zangu na mtu Yule anayeishi aina
mbili za
maisha [wokovu na dhambi].” Akaanza kunionesha watu wanaoelekea kuzimu.
Walikuwa
wamefungwa kamba toka mikononi hadi miguuni. Kila mmoja alivaa vazi jeupe,
lakini
limetobokatoboka, lina-mabakamabaka na limekunjamana. Yesu akaniambia, “Binti,
angalia watu
walioniacha mimi. Binti, nataka kukueleza, siji duniani kwaajili ya watu hawa.
Nakuja kwaajili
ya watakatifu, waliotayari, wasiolaumiwa, wasio na makunyanzi na wasio na
mawaa…… nenda
uwaambie warejee kwenye njia zao za zamani,” (Efeso 5:26-27) Nilianza kuwaona
wengi
miongoni mwa wajomba zangu na watu wengine wengi waliorudi nyuma na kuziacha
njia za
Bwana. “Nenda kawaambie ninawasubiri, walete mizigo yao nami
nitawapumzisha." YESU
alikuwa analia baada ya kusema hayo, “Binti, wanakuja huku [kuzimu]. Nenda
kawaambie
wajomba zako; nenda kawambie ndugu zako kuwa wakuja huku! Binti, wengi
hawatakuamini,
lakini mimi ni shahidi wako mwaminifu, ni shahidi wako mwaminifu. Sitakuacha
wewe. Hata
kama hawataamini, Binti, nenda na uwaambie ukweli huu, kwa kuwa nipo nawe. Pia
Binti
nitakuonesha jinsi watu wanavyofika huku.”
Tulikwenda kwenye lango, ambapo tuliona umati wa watu wakiangukia ndani ya
shimo kubwa.
Siyo elfu moja wala elfu mbili, bali wingi wake kama mchanga wa bahari, hawana
idadi!
Walikuwa wananguka kwa kila sekunde, mfano wa mkono uliojaa mchanga umwakikapo
chini.
Zile roho zilikuwa zinaanguka kwa kasi. YESU alikuwa akilia, na kusema, “Binti
hivi ndivyo
wanadamu wanavyopotea; hivi ndiyo mwanadamu apoteavyo!!!..... Binti, inaniumiza
sana mimi
nionavyo wanadamu wanavyoangamia.”
YESU akasema, “maapepo pia hufanya mikutano huku.” Na nikasema, “mapepo
yanafanya
mikutano?” Yesu akasema, "Ndiyo, Binti, wanakutana kupanga, kupanga
watavyowafanya
wanadamu. Wanakutana kila siku kwa siri.” Na kwa hilo, Yesu akanipeleka kwenye
sero,
ambapo niliona meza ya mbao na viti vikizunguka meza. Na palikuwa na mapepo,
aina zote za
mapepo. Yesu akaelezea, “Binti, wanapanga kwenda kuharibu nyumba/familia za
wachungaji,
wamisionari, wainjilisti na wote wanijuao mimi. Binti wanataka kuwaharibu;
wanamishale
mingi.”
Mapepo hucheka na kudhihaki, na kusema, “acha tuwaharibu wanadamu na kuwaleta
huku.” Yesu
akasema, “Nenda na uwaambie nipo pamoja nao watu wangu. Waambie wasiache
milango wazi,
wasimpe nafasi shetani, kwa kuwa shetani anazunguka-zunguka kama simba
angurumaye,
akimtafuta wa kummeza. (1 Petro 5:8)" Lakini neno linasema,
"anatembea kama", kwasababu
simba halisi, ni Simba wa Yuda, Yesu Kristo wa Nazareti (Ufunuo 5:5)! Yesu
akasema, "Binti,
wanataka kuharibu/kuangamiza familia za wachungaji.” Nikamuuliza, “Kwanini
wanataka
kuharibu familia za wachungaji?” na Yesu akajibu, “Kwasababu wanawajibu wa maelfu
ya watu
ambao ni kondoo wa kundi; kondoo wa kundi Bwana aliowakabidhi wao. Wanataka
watu hao
warudie dunia tena; waangalie nyuma na kuishia kuzimu…. Nenda kawaambie
wachungaji
kusema iliyo kweli tupu. Waeleze wahubiri kweli tupu na kusema kila kitu ninachowaambia
na
wasinyamaze nayo haya ninayowaambia!”
Tulipokuwa tunaondoka hapo, akaniambia, “Nataka nikuoneshe kitu kingine…. Wapo
pia watoto
huku.” Na nikamjibu, “watoto huku Bwana? Kwanini wawepo watoto huku? Neno lako
lasema,
'Waacheni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie: kwa maana Ufalme wa Mbinguni
ni wao."
(Mathayo 19:14) Yesu akajibu, “Binti, ni kweli, ufalme wa mbinguni ni wao,
lakini mtoto lazima
aje kwangu, kwa kuwa kila ajaye kwangu sitamtupa kamwe." (Yohana 6:37)
Ghafla, Bwana
akanionesha mvulana wa miaka nane akiteswa kwenye moto. Mvulana akalia, “Bwana
nihurumie
mimi, nitoe mahali hapa, sitaki kuwepo hapa!” aliendelea kupiga kulia na
kelele. Nikaona mapepo
yamemzunguka mtoto huyu, yaliyofanana na cartoon. Kulikuwa na aina za Dragon,
BoyZ, Ben 10,
Pokémon, Doral, na nyingine nyingi. “Bwana, kwanini mtoto huyu yuko huku?"
Yesu akanionesha
picha ya mkanda wa maisha mtoto huyu. Nilimwona anavyotumia muda karibia wote
kwenye
LUNINGA [TV] akiangalia cartoon.
Cartoon ya Ben 10: Pokemon:
Yesu akasema, "Binti, hayo maigizo ya cartoon, sinema zake, michezo
mbalimbali ya kuigiza
inayooneshwa kila siku kwenye LUNINGA [TV] ni vyombo vya shetani atumiavyo
kuwaharibu
wanadamu….. tazama, binti ilivyotokea kwa mtoto huyu." Nilimwona jinsi
mtoto huyu
alivyokuwa mkaidi na asiye mtii kwa wazazi wake. Wazazi wake aliposema naye
alikimbia na
kutupatupa vitu ovyo na kuto-watii. Baada ya hapo akagongwa na gari na ukawa
mwisho wa
maisha yake. Yesu akasema, “Tangu hapo yupo mahali hapa.”
Nilimtazama mtoto Yule akiteswa. Yesu akasema, "Binti, nenda na uwaambie
wazazi
wawaelekeze watoto wao kama ilivyo katika neno langu.”(Mithali 22:6) Neno la
Mungu ni halisi,
linatuambia tumwonye mtoto kwa fimbo, lakini si kila wakati, pale tu mtoto
anapoonyesha ukaidi
kwa wazazi. (Mithali 22:15)
Bwana akaniambia kitu cha kuhuzunisha sana na kuumiza mno. Akasema, “Binti,
wapo watoto
wengi sana huku kwasababu ya cartoon, kwasababu ya ukaidi.” Nikamuuliza,
“Bwana, kwanini
lawama ziwe hizi cartoon?” Naye akanieleza, “Kwasababu ni mapepo yanayobeba
ukaidi, kiburi,
ukali na chuki kwa watoto, ili wasifanye vitu vizuri; na mapepo mengine
huwaingia watoto ili
wasifanye mambo mazuri, bali wafanye mabaya: vile waonavyo kwenye LUNINGA [TV]
watoto
hutaka kufanya vivyo hivyo.” Kuzimu ipo, kuzimu ni halisi, na watoto lazima
waamue
watakwenda na nani. Nikasema, “Bwana, niambia, kwanini kuna watoto huku?” na
Yesu akanijibu,
“Mara watoto wapatapo kujua kuna mbinguni na kuzimu, hapo wanayonafasi ya
kuchagua.”
UFALME WA MBINGUNI
Kuna mengi ya kusema juu ya kuzimu, lakini kwasasa niwashirikishe niliyoyaona
Mbinguni. Yesu
akasema, "Binti, sasa nitakuonesha nilichowaandalia watakatifu wangu.”
Tuliondoka kule
kuzimu kupitia lango lake. Tulipokuwa tukisafiri kutoka nje ya kuzimu, ghafla
tukatokea mahali
penye mwanga. Sikuona giza tena, mateso wala miale ya moto. Akasema, “Binti,
nitakuonesha
utukufu wangu,” na tukaanza kupanda juu kwenda Ufalme wa Mbinguni! Mara
tukafika kwenye
mlango wenye maandishi makubwa yaliyoandikwa kwa dhahabu, yalisema: “Karibu
kwenye Ufalme wa Mbinguni.”
LANGO LA MBINGUNI
Yesu akasema, “Binti, ingia, kwa kuwa mimi ni Mlango na kila aingiaye kupitia
kwangu,
ataingia na kupata marisho.”(Yohana 10:9)
Baada ya Bwana kusema maneno hayo, mlango ukafunguka na tukaingia. Niliwaona
malaika
wakimpa utukufu, heshima na sifa Baba Yetu wa Mbinguni! (Ufunuo 7:11-12) Kadri
tulivyozidi
kutembea, tulikaribia meza niliyoweza kuona mwanzo wake laini siyo mwisho.
(Ufunuo 19:9)
Niliona enzi kubwa, na enzi ndogo zimezungukwa na maelfu ya viti. Katikati ya
viti niliona mavazi
na mataji. Bwana akaniambia, “Binti, taji unayoiona pale ni taji ya
Uzima."(Ufunuo2:10)
Yesu akasema, “Tazama, Binti, hii ndiyo niliyowaandalia watu wangu.” Niliona
ile meza
imefunikwa na vitambaa vyenye upindo wa dhahabu. Kulikuwa na sahani, glasi za
dhahabu,
matunda; kila kitu kimeandaliwa. Ilikuwa nzuri ajabu. Kulikuwa na chombo
kikubwa katikati ya
meza, kilichokuwa na mvinyo tayari kwa mulo. Na Yesu akasema, “Binti, kila kitu
kipo tayari kwa
ujio wa kanisa langu.”
MEZA YA KARAMU YA MBINGUNI
Tulikwenda mahali pengine, niliwaona watu wengi wakiwa bustanini. Kulikuwa na
watu
wanaofahamika sana kwenye Biblia, lakini hawakuwa wazee, bali vijana. Palikuwa
na kijana akiwa
na kitambaa mkononi, akicheza na kuzungukazunguka na kumsifu Bwana. Yesu
akasema, “Binti,
Yule kijana pale ni mtumishi wangu Daudi.” Alikuwa akimpa utukufu Baba yetu.
Ghafla, kijana
mwingine akapita na Yesu akaniambia, “Binti, huyu ni Joshua; Yule Musa; na Yule
pale ni
Ibrahimu.” Yesu huwaita kwa majina yao. Wote walikuwa na mwonekano mmoja! Ajabu
sana
Mbinguni! Yesu akasema, “Mwanamke Yule ni mtumishi wangu, Maria Magdalena; na
Yule
mtumishi wangu Sara."
Lakini pia akaniambia, “Binti, huyu ni Maria. Maria, aliyemzaa Yesu Kristo,
ambaye ni mimi.
Binti, nikwambie, yeye hana habari ya yanayotokea duniani. Nataka kukwambia,
nenda
kawaambie wanadamu, waambie waabudu sanamu kuwa kuzimu ni halisi, na waabuduo
sanamu hawata urithi Ufalme wangu, lakini waambie kama wakitubu, wataweza
kuingia makao
ya mbinguni. Nenda waambie nawapenda na pia waambie Maria hajui chochote
[kinachotendeka duniani] na pekee wanayeweza kuheshimu ni mimi, kwasababu si
maria wala
mtakatifu Gregory wala mtakatifu yeyote awezaye kuokoa. Mimi ndiye niokoaye na
nje yanguhakuna
yeyote, hakuna yeyote, hakuna yeyote – aokoaye!” Alirudia mara tatu-kuwa hakuna
yeyote awezaye kuokoa; isipokuwa yeye.
Wanadamu wamedanganywa na kuamini kuwa kwa kupitia wadhaniwao ni watakatifu,
sivyo
ilivyo, bali ni mapepo, yafanyayo kazi kupitia sanamu zilizofanywa kwa mikono
ya watu. Lakini
ngoja nikueleze kwamba Bwana anataka kukupa kilicho bora. Anataka wewe uingie
katika Ufalme
wa Mbinguni; tubu na kuacha uabudu sanamu. Kwasababu ibada ya sanamu
haitakuokoa wewe.
Yesu Kristo wa Nazareti ndiye pekee aokoaye, aliyeutoa uhai wake kwaajili yako,
yangu na
kwaajili ya wanadamu wote. Bwana ana ujumbe mzito kwa wanadamu. Huku akilia
aliniambia,
“Tafadhari, Binti, usikae kimya; nenda na uwaambie ukweli, nenda na uwaambie
nilichokuonesha wewe.”
Sanamu za Maria na Waumini wa kisujudia
Nilimwona Maria akimwabudu Bwana, na niliwaona wanawake wakiwa na nywele ndefu
nzuri.
Nikasema, “Bwana, wanapendeza sana walivyoweka nywele zao.” Akaniambia, “Binti,
kile
uonacho ni utaji niliowapa wanawake.” Akaongeza, “Binti, nenda na uwaambie
wanawake
watunze utaji niliowapa.”
Kisha akaniambia, “Nina kitu cha muhimu cha kukuonesha.” Nikatazama mbali
kidogo na kuona MJI UNG’AAO, MJI WA DHAHABU! Nikasema, “Bwana, kile ni nini?
Nataka kwenda pale.” Akanijibu, “Binti, nitakuonesha kilichopo pale. Ukionacho
ni makao ya Mbinguni, majumba ya Mbinguni yaliyotayari kwaajili ya watu wangu.”
Tulianza kutembea, hadi tukafika kwenye daraja la dhahabu. Mara tulipovuka
daraja, tukafika kwenye mitaa iliyotengenezwa kwa dhahabu safi! (Ufunuo 21:21)
Kila kitu kilikuwa kizuri sana, kuzuri sana pale, kunang’aa kama kioo, ni
mahali pasipo pakawaida, hakuelezeki! Tuliona majumba ya ki-mbinguni na pia
tuliwaona, maelfu ya malaika wakijenga. Baadhi ya malaika walikuwa wanajenga
kwa haraka ya ajabu, na wengine pole pole na wengine walikuwa wamesimama kabisa
kujenga. Nikamuuliza Bwana, “Kwanini malaika wengine wanajenga haraka haraka,
wengine polepole, na wengine wamesimama?" Bwana akanieleza, “Binti, hivyo
ndivyo wafanyavyo watu wangu duniani, na malaika wanafanya kama wafanyavyo watoto
wangu duniani…. Binti, watu wangu hawahubiri neno langu. Watu wangu hawafungi
tena. Watu wangu hawaendi mtaani kusambaza ujumbe wa neno langu kwa vipeperushi
vinavyoeleza ukweli. Watu wanaona aibu kuhubiri. Nenda kawaambie watu wangu
warudi kwenye njia za zamani. Wale malaika uliowaona hawafanyi chochote ni
malaika wa watu wangu waliorudi nyuma na kuacha njia zangu… Binti, nenda
waambie watu wangu warudi njia zao za zamani,” (Yeremia 6:16) na baada ya
kusema haya akaanza kulia Bwana.
Nikasikia watu wengine wakiimba, hivyo nikamuuliza, “Bwana, nataka unipeleke
kule, ambako watu wanaimba.” Yesu alikuwa akiniangalia, nakwambia jinsi
alivyokuwa ananiangalia, sikuweza kuona vema uso wake bali alikuwa akigeuza uso
wake. Wakati huo machozi yalikuwa yakimtiririkia kwenye vazi lake, nikamuuliza
kwanini analia. Lakini hakuweza kunieleza.
Baadaye tulifika kwenye bustani nzuri sana. Pale katika majumba ya mbinguni,
niliona maua yalikuwa yakiyumbayumba huku na huku kama yapulizwayo na upepo.
Hizi huenda ndizo sauti za kuimba nilizozisikia. Bwana akaninyoshea kidole na
kusema, “Binti, tazama, maua yananisifu mimi; yananiabudu mimi! Watu wangu
hawafanyi hivi tena kama walivyokuwa wanafanya mwanzo. Watu wangu hawanisifu,
hawaniiabudu mimi; hawanitafuti mimi kama mwanzo. Ndiyo maana nalikwambia
mwanzo, Binti, nenda na uwaambie watu wangu wanitafute, kwa kuwa nitakwenda,
nitakwenda, nitakwenda kwa wanaonitafuta kwa roho na kwa kweli, kwa watu walio
tayari, kwa watakatifu!” na huku akilia akasema, “Ninakuja, ninakuja!” hapo
nikaelewa kwanini alikuwa analia, kwasababu anakuja, lakini si kwa wasio na
nia, watu wa nia mbili [vuguvugu]. Atarudi kwa wale tu wanaomtafuta katika roho
na kweli.
Ndipo Bwana akaniambia ninatakiwa kurudi duniani. Nikasema, “Bwana, Sitaki
kurudi duniani! Unamaanisha nini- duniani? Nataka kubaki na wewe Bwana.
Umenileta huku na mimi siendi kokote kwasababu niko na wewe!”
Yesu akasema, “Binti, ni muhimu urudi duniani ili ukashuhudie kwamba utukufu
wangu ni halisi, yote niliyokuonesha kuwa ni kweli; ili wanadamu waje kwangu,
watubu na wasiangamie.” Bwana akaanza kulia, nami nikaanguka miguuni pake;
nikaona vidonda kwenye miguu yake. Nikamuuliza, “Bwana, hivi ni vidonda vya
nini?” akajibu, “Binti, ni vidonda ya jana, nilipotoa maisha yangu kwaajili ya
wanadamu.”
MKONO WA YESU
Bwana akanionesha vidonda vyake vya mikononi, nilimuuliza, “Bwana, kwanini
ungalinavyo hata
sasa?” akaniambia, “Binti, ni vidonda vilivyobaki.” Hivyo nikamuuliza, “je
vitapona?” akanijibu,
“Vitapona na kufutika tu baada ya watakatifu wote kuungana hapa….. Binti,
lazima
nikurudishe duniani: Familia yako na mataifa yanakusubiri wewe.”
Nilijaribu kukataa lakini akanyosha kidole chake chini duniani na kusema,
“Tazama, wale watu
uwaonao chini pale ni ndugu zako; na mwili ule uuonao pale, ndiyo utakaoingia……
ni muda
wa kuondoka mahali hapa.” Baada ya hapo akaanipeleka kwenye mto mzuri mwangavu
na
akasema, “Binti, ingia katika mto na jizamishe mwenyewe.” Kabla sijaingia ndani
ya mto wa maji
ya uzima, nilikuwa najisikia furaha ya ajabu, lakini baada ya kujizamisha na
kutoka nje, nilipata
furaha kuu. Nilidhani sitarudi tena nyumbani kwetu, lakini Bwana akaniambia,
“Binti, unatakiwa
kurejea duniani….. Binti, nitakuonesha kitu: jinsi nitakavyorudi mara ya pili
kwaajili ya watu
wangu watakatifu. Nitakuonesha jinsi siku ile ya kutisha itakavyokuwa.”
FURAHA NA MAOMBOLEZO
Tulitembea hadi sehemu yenye kioo kikubwa kama LUNINGA [TV], nikaona watu.
Niliweza
kuona dunia yote. Ghafla nikaona maelfu ya watu wakipotea. Wanawake wenye
mimba, mimba
zilipotea, na wakawa kama wamechanganyikiwa na kupiga mayowe.
Watoto walitoweka pande zote. Watu wengi walikuwa akikimbia huko na huku,
wakipiga kelele,
“Haiwezekani, haiwezekani, nini hiki kitokeacho?”
Niliwaona wale waliomjua Bwana na kuachwa nyuma. (Mat.24:40-41) Walikuwa wakisema
Kristo
amekuja, furaha imetimia. Walikuwa wakipiga kelele na kutafuta kujiua wenyewe
lakini
hakuwezekana. Bwana akaniambia, “Binti, siku hizo kifo kitawakimbia; Binti,
siku hizo Roho
Mtakatifu hatakuwepo tena.” (Ufunuo 9:6) kulikuwa na ajali nyingi lakini
sikuona hata mtu
mmoja aliyekufa: wote walikuwa wazima japokuwa wameumia [majeruhi].
Niliona mlolongo mrefu wa maelfu ya watu. Akaniambia, “Binti, tazama, hivi
ndivyo kila kitu
kitakavyokuwa.” Kisha nikaona watu wakikimbia kutoka sehemu moja kwenda nyingine,
wakipiga
kelele, Kristo kaja, Kristo kaja!” wakisihi, “Bwana nisamehe mimi, nisamehe
mimi, nichukue
nawe!”
Baada ya Bwana kuwachukua watu wake [Unyakuo]
Lakini kwa huzuni Bwana akasema, “Watakuwa wamechelewa. Muda wa kutubu ni
sasa…. Binti,
nenda kawaambia wanadamu wanitafute mimi, wakati huo hakutakuwa na nafasi.
(Isaya 55:6)
Binti, watakuwa wamechelewa wote watakaobakia nyuma.” Baada ya Yesu kuona watu
wataobaki nyuma akaanza kulia na kusema, “Binti, nitakwenda duniani kama neno
lisemavyo
katika 1 Thes. 4: 16-17: “Kwasababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni
pamoja na
mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika
Kristo
watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao
katika mawingu,
ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi
farijianeni kwa
maneno hayo.”
SIKU YA MWISHO
Lakini si kila mtu atakwenda na Bwana, wale tu wafanyao mapenzi yake (Mathayo
7:21) na aishiye
maisha matakatifu. Kwa kuwa Bwana aliniambia, “Wale tu walio watakatifu
wataoingia Ufalme
wa Mbinguni, (Waebrania 12:14) Hakuna ajuaye, siku wala saa nitakayokuja
kwaajili ya watu
wangu watakatifu, hata malaika hawajui.” (Mathayo 24:36)
Kwenye Kioo cha LUNINGA [TV] niliona watu wakikimbia huko na huku. Magazeti
yalisema
“KRISTO AMEKUJA.” Kioo kikafungwa, na Yesu akamalizia kwa kusema, “Ninakuja kwa
watakatifu.” Hivi ndivyo alivyonionesha mimi. Baada ya hapo akanirudisha
duniani hapa. Tukiwa
na kusanyiko la malaika wengi wakituzunguka, tulianza kushuka ngazi nzuri kama
nini; ngazi
nyeupe na maua yakizunguka. Nilikuwa nalia njia nzima kushuka chini, nikimsihi
Yesu, “Bwana
tafadhari usiniache hapa. Nichukue niwe nawe!” Alinijibu, “Binti, mataifa
yanakusubiri,
familia yako wanakusubiri wewe…….. Binti, lazima urejee mwili wako. Lazima
upokee uhai
wako, Binti, ili uweze kwenda kushuhudia yote uliyoyaona. Wengi hawatakuamini
wewe; wengi
watakuamini, bali mimi ni shahidi wako mwaminifu. Niko pamoja nawe. Sitakuacha
kamwe."
KURUDI DUNIANI KWA ANGELICA
Maxima:
Binti yangu aliporudi, tulikuwa tunamsubiri pale, na alikuwa amelazwa pale pale
chini sakafuni.
Nikasikia mguno, "uuhmm," bila kitu. Nikasema, “ahsante Bwana
kwasababu Binti yangu
amerudi!”
Sote tulimshukuru Bwana. Mara akaanza kupumua polepole, kidogo kidogo. Baada ya
muda wa
masaa matano, alikuwa na uwezo wa kufumbua macho na kusema. Mwanzo tulipata
shida
kumuelewa asemacho; ilikuwa ni vigumu kumuelewa. Hakuwa na nguvu kabisa.
Ilibidi tufunge
madirisha kwasababu macho yake hayakuwa na uwezo wa kuhimili mwanga.
Kwakuwa wadadisi, sote tulitaka atueleze alichoona. Lakini kwa kuwa alikuwa
dhaifu, aliweza
kutueleza kidogo tu. Ilimchukua karibu wiki mbili hadi alipoweza kutushirikisha
habari nzima ya
ushuhuda wake.
Mapepo yalikuja kumtesa baada ya hayo yote. Aliweza kuyaona waziwazi;
yalijaribu kujificha
kwenye vivuli. Yalikuwepo hapa karibu siku tatu mfululizo tangu arudi, kabla
hajaweza kutueleza.
Aliyauliza yalikuwa yanataka nini, nayo yakamjibu, “tumekuja kufanya mkataba
nawe……. Ni
lazima ufunge mdomo, ni lazima usiseme lolote ya hayo uliyaona kule chini,
kwasababu ukisema,
tutakuuwa.” Aliyaelezea yalivyo mapepo, yana sura mbaya, makubwa na manene
yanatisha.
Alisema hakuna maneno yakuelezea jinsi yatishavyo kwa mwonekano. Alijaribu
kuyakemea lakini
yalikataa kuondoka. Yakifika yalikuwa yanamrukia na kumchoma. Naye aliendelea
kupambana
nayo na kuyakemea, lakini hakuweza kwasababu hakuwa na nguvu. Siku moja
alipokuwa
anayakemea, mwanga mkali wa ajabu ulitokea na yakakimbia yote! Alikuwa ni
Bwana.
Alichopitia Binti yangu hakikuwa rahisi. Alipewa ujumbe wenye maono ya ndani
kwaajili ya
wanadamu, ili wamtafute Mungu. Wanadamu wanadhani wafanyayo ni sahihi. Vijana
wamezama
kwenye madawa ya kulevya na pombe, na kuona ni sawa maisha hayo, lakini si
sawa. Miongoni
mwa alioneshwa binti yangu ya kutisha ni wasanii wengi walivyojaa kuzimu,
wanamuziki/wacheza
dansi na pia Papa John Paul II. Ni wakati wa kumtafuta Bwana, kutubu, na
kujishusha na kujidhiri
mbele za zake. Neno la Mungu ni kweli lisemalo, “Mbingu na nchi zitapita;
lakini maneno yangu
hayatapita kamwe.”(Mark 13:31) Neno la Bwana litatimizwa katika muda wake.
Bwana
alimwonesha tanuru ambalo watu walikuwa wanatembea kuelekea kuzimu. Na watu
wengi tayari
wakiwakuzimu. Ni kweli haya, lakini hata watu wa Mungu hawaamini haya, wengi
hawaamini.
Ujumbe mkuu ni kwamba tumtafute Bwana, siyo kwa kinywa/mdomoni, bali kutoka
ndani ya
moyo, kwakuwa kurudi kwa Bwana ku-karibu. Yesu alisema, “Siko tena mlangoni;
niko zaidi ya
mlangoni. Nakuja muda simrefu; kuja kwangu ku-karibu. Watu wangu wameniacha na
wamerejea mambo ya duaniani……… waambie watu wangu warudie njia zao za zamani.”
Kanisa leo linatakiwa kurudia njia zake za zamani; hapa tulipo ni wa motoni,
tumtafute Bwana.
Pale parapanda ikilia tuwe tayari kukutana na Bwana, itakuwa ajabu sana!
UJUMBE WA MUHIMU WA BWANA
Angelica akiongea mbele ya haraiki:
Bwana akaniambia, “Binti, siku hizo Roho Mtakatifu hatakuwepo tena duaniani.
Siku hizo
hatakuwepo duniani.” (2 Thes. 2:7) Na nikaona msongamano mkubwa wa magari na
ajali nyingi
sana. Watu wengi walijaribu kujiua, lakini Yesu akasema, “Watatafuta kifo,
lakini kifo
kitawakimbia wanadamu. Kifo hakitakuwepo tena siku hizo.”(Ufunuo 9:6) Nikawaona
watu
wakitazama LUNINGA [TV] na kusoma magazeti yakisema, “Maelfu na maelfu wamepotea.”
Wengi watajua kuwa Yesu ameshakuja kwaajili ya watu wake watakatifu. Wale
waliomjua Bwana
lakini wameachwa, wakakimbia mitaani wakilia, wakijaribu kujiua wenyewe lakini
hawakuweza
lolote.
Nilipokuwa mbinguni, Yesu alisema, “Nina kuja duniani kwaajili ya watu wangu
watakatifu na
ninakuja mapema kwaajili ya kanisa langu.” Lakini wiki mbili zilizo pita Bwana
aliniambia,
“Binti, ninafurahishwa na unavyotenda, kwa kuwa unatimiza niliyokuagiza na
nakukupa, lakini
usiwaambie watu wangu kuwa nitakuja mapema, waambie ninakuja sasa hivi.” Tena
Bwana
akasema, “Waambie watu wangu ninakuja sasa hivi na ninakuja kwa watu
watakatifu. Waambie
watu wangu nakuja kwa watakatifu tu, nao ndio wataoniona mimi!.... tena
usinyamaze: endelea
kuwashuhudia ninayokwambia.”
Angelica akiomba na haraiki:
Kila mmoja afumbe macho, na weka mkono wako wa kuume kifuani. Inua mkono wa
kushoto juu,
kama unajisikia kulia[toba], lia tu. Sasa mweleze Bwana kile unachojisikia
moyoni. Kwa wale
waliotayari kumpokea Bwana, wafuatiane nami ktika maneno haya:
Bwana, ninakushukuru kwa Upendo na huruma yako, ahsante Bwana kwa maneno yako
yaliyotufikia mioyoni leo. Baba, ninaomba msamaha kwako, unisamehe. Unisamehe
mimi.
Unioshe kwa damu yako ya thamani. Andika jina langu katika kitabu cha uzima.
Nipokee/nikubali
mimi niwe mwanao Bwana. Sasa hivi, ninamsamehe kila mtu niliyeshindwa
kumsamehe. Ninakana
hali yangu ya kutosamehe. Ninayakana yote yalinizuia nisikufuate Bwana,
ninaomba unibadilishe
Bwana na unijaze uwepo wako ndani yangu kila siku. Ahsante Baba, Mwana, na Roho
Mtakatifu,
Ameni.
Angelica:
Ushuhuda huu siyo uwongo; siyo mzaha; siyo hadithi; siyo ndoto, kuzimu ni kweli
ipo! Kuzimu ni
halisia! Kwa yeyote asiyeamini, nataka kukueleza kuzimu ni kweli ipo, ni kweli
ni halisi. Ninakosa
maneno zaidi mazuri ya kuelezea uhalisia wa kuzimu. Natamani kama ungeshuhudia
wewe
mwenyewe. Lakini tafadhari amini, tii na uonyeke kwa ushuhuda huu [ushuhuda
ukuonye na
kukubadilisha] ili uepuke moto wa milele.
Angelica akiongea na Mfasiri/Muelezeaji:
Muda ukaribu sana, Mungu anaruhusu ishara kwa wanadamu zitokee ili kuwaonesha
kitakachotokea. Usibakie ukihukumiwa; ndilo shetani atakalo. Jiulize kama uko
tayari ukitembea
kuelekea shimo la kuzimu? Leo ni siku ya wokovu, leo ni siku ya kumkaribisha
Yesu, kuwa Bwana
na mwokozi wa maisha yako. Haya ni maneno rahisi lakini ni makubwa sana kusema:
“Ninakubali
na kukupokea Yesu uwe Bwana na Mwokozi wangu. Ninakupa wewe maisha yangu na
roho yangu
kwa moyo wangu wote. Natakuwa kuwa nawe kwa maisha ya milele.”
Chagua hatima yako baada ya maisha haya: Uzima au mauti, Mbinguni au kuzimu,
Yesu au
shetani. Iko wazi, uko upande wa Yesu au upande wa shetani. Au unafanya yaliyo
mema au
unafanya yaliyo mabaya. Chagua mwisho wako: uzima wa milele au ziwa la moto.
Fikiria jambo
hili. Fanya uamuzi sasa. Yesu Kristo alikufa msalabani kwaajili yetu, kwa
dhambi zetu, na akatupa
fursa ya wokovu kwa huruma yake. Mpokee Yesu Kristo kuwa mwokozi wako!
“Sasa umesikia ushuhuda huu, usiipoteze nafasi hii
ukaijutia milele na milele motoni.”
Marejeo:
Ufunuo 19:9 ….Heri walioalikwa karamu ya arusi ya mwanakondoo. ……..maneno haya
ni maneno ya kweli ya Mungu.
Ufunuo 20:15 Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha
uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Ufunuo 21:4 Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwepo
tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwepo tena; kwa kuwa
mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Ufunuo 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza
na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
Ufunuo 21:8 Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na
wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa
liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
“Hakuna waabuduo sanamu wataourithi ufalme wa Mbinguni.”
Kutoka 20:4-5 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote
kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya
dunia. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni
Mungu wenye wivu……..
Ufunuo 21:21 Na milango kumi na miwili ni lulu kumi na mbili; kila mlango ni
lulu moja. Na njia ya mji ni dhahabu safi kama kioo kiangavu.
Ufunuo 21:27 Na ndani hakitaingia kamwe chochote kinyonge, wala yeye afanyaye
machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha mwana
koondoo wa Mungu.
Ufunuo 22:7 Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa
kitabu hiki.
Ufunuo 22:11 Mwenye kudhuluma na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi
kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi
kutakaswa.
Ufunuo 22:12 Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu
kama kazi yake ilivyo.
Ufunuo 22:13-15 Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa
mwisho. Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri ya kuuendea huo mti wa uzima, na
kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na
wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
Ndugu aliyefasiri ufunuo huu ni Alpha Wilson Magubila ni Mwana UWATA (Uamusho
Wa Wakristo Tanzania); Jumuiya iliyosajiriwa na Yenye Msingi wa Kutubu Dhambi
na kuziacha (Mithali 28:13). Waebrania 6:4-6, 2Petro 2:20-22.